#Local News

KERRA: MHASIBU KORTINI KWA TENDA ZA UFISADI

Katika juhudi za kupiga vita ufisadi nchini, mhasibu msaidizi wa KeRRA, Esther Wanjiru Chege, amefikishwa mahakamani Kajiado pamoja na washukiwa wawili kwa tuhuma za kutoa tenda za serikali kwa kampuni zinazohusishwa na mumewe.

Kwa mujibu wa EACC, Wanjiru alitumia nafasi yake vibaya, akitoa kandarasi kwa kampuni tatu za mumewe, huku pia akimiliki mali isiyolingana na kipato chake halali.

Washukiwa walikamatwa Mei 2, 2025, na wameshtakiwa kwa makosa ya mgongano wa maslahi, ununuzi haramu wa mali ya umma, na njama ya kutenda uhalifu wa kiuchumi. Walikana mashtaka na kesi hiyo itaendelea Mei 9, 2025.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *