KPCA YAOMBA KUJUMUISHWA UONGOZI WA BODI YA KAHAWA

Mwakilishi wa wakulima katika Chama cha wakulima wa kahawa nchini eneo la Bungoma Kanali mstaafu Tom Wanambisi, amepongeza hatua ya serikali kufutilia mbali deni la wakulima hao la shilingi bilioni 6.8, na kumtaka Rais William Ruto kuhakikisha kuwa madeni ya kila mkulima pia yanafutiliwa mbali.
Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi, Wanambisi amesema hatua hiyo itawawezesha wakulima kuendelea kukumbatia zao hilo ambalo kwa muda limekumbwa na changamoto.
Aidha, Wanambisi ameomba bunge la kitaifa na lile la seneti kuhakikisha kuwa yanatengeneza sheria zitakazoleta mageuzi katika sekta ya kahawa, ikiwemo kushirikisha wakulima wa kahawa katika bodi ya zao hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa