ASANTENI SANA

Mshindi wa nishani ya shaba katika mbio za marathon za wanawake Hellen Obiri amewashukuru Wakenya kwa uungaji mkono ambao wamewapa timu inayowakilisha taifa kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris.
Katika taarifa yake baada ya kuibuka nambari tatu katika mbio za marathon za Olimpiki za Paris kwa wanawake, Obiri alibainisha kuwa Kenya imefunga Olimpiki kwa medali 11.
Jumapili asubuhi, Obiri alikamilisha mbio za kilomita 42 kwa muda wa saa 2.23.10, nyuma ya Sifan Hassan wa Uholanzi (2.22.55) na Tigist Asefa wa Ethiopia (2.22.58) na kushindia Kenya medali ya kumi na moja katika mashindano hayo.
Imetayarishwa na Nelson Andati