#Football #Sports

BAADHI WACHEZAJI WA ASENALI WAKUMBWA NA MAJERAHA

Baadhi ya wachezaji wa timu ya arsenali wanakumbwa na majeraha kadhaa ambayo yamesababishwa na mechi za taji la UEFA nations league.

Wana gunners wamepata pigo baada ya baadhi ya wachezaji wao kulazimika kuukosa mchuano dhidi ya Tottenham Hotspurs na Manchester City.

Wachezaji hao ni pamoja na Mikel Merino, Declan Rice mzaliwa wa uingereza ambaye alionyeshwa kadi nyekundu wakati wa mechi yao na Brighton, beki, sajili mpya Riccardo Calafiori ambaye alipata jeraha akichezea timu yake ya taifa Italia, na Martin Odegaard ambaye vile vile anatazamiwa kuwa nje kwa angalau wiki tatu kutokana na jeraha la mguu akichezea timu ya taifa ya Norway.

Hii ni ishara kuwa kocha wa arsenali Mikel Arteta atakuwa na kibarua kigumu kudhibiti makali ya wana Hotspur siku ya jumapili.

Arsenali kwa sasa wana pointi saba baada ya kulazimisha sare dhidi ya Brighton. Baada ya kucheza na Tottenham Hotspurs, arsenali watakuwa wageni wa city ambao hawajapoteza mchuano hata mmoja tangia msimu wa 2024/2025 kuanza, huku wakiongoza jedwali ya ligi kuu ya uingereza.

Imetayarishwa na Osoro Kennedy

BAADHI WACHEZAJI WA ASENALI WAKUMBWA NA MAJERAHA

TIMU YA FIRAT KUONYESHA MAKALI YAKE DHIDI

BAADHI WACHEZAJI WA ASENALI WAKUMBWA NA MAJERAHA

TETESI ZA UHAMISHO- SOKA ULAYA MSIMU HUU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *