#Sports #Tennis

SINNER AFIKA FAINALI

Mchezaji nambari moja duniani Jannik Sinner amefika nusu fainali yake ya kwanza ya US Open kwa ushindi wa seti nne za 6-2, 1-6, 6-1, 6-4 dhidi ya bingwa wa 2021 na mshindi wa pili mara mbili Daniil Medvedev.

Sinner sasa atamenyana na Jack Draper wa Uingereza kutinga fainali.

Sinner, 23, ndiye mchezaji pekee wa 10 bora aliyetinga nusu fainali akiwa na nambari 12 Taylor Fritz ambaye atamenyana na raia wa Marekani, Frances Tiafoe, aliyeorodheshwa wa 20, katika pambano lingine la nusu fainali kesho.

Sinner wa Italia alikuwa amemshinda Medvedev na kunyakua taji la Australian Open, kabla ya Mrusi huyo kulipiza kisasi kwenye Wimbledon.

Imetayarishwa na Nelson Andati

SINNER AFIKA FAINALI

SUDAN YASHINDA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *