PIGO MAHAKAMANI KUFUATIA KIFO CHA JAJI SIAYA

Idara ya mahakama imepata pigo jingine baada ya Jaji wa mahakama kuu ya Siaya Daniel Ogola Ogembo kuaga dunia, siku chache baada ya mwenzake David Majanja kuaga dunia.
Mwili wa jaji Ogembo umepatikana nyumbani kwake asubuhi ya leo, polisi wakisema wamefahamishwa kuhusu kifo chake na dereva wake aliyekuwa amekwenda kumchukua kumpeleka kazini ilivyo kawaida.
Imearfiwa kwamba jaji huyo alikuwa pekee yake nyumbani kwake alipofariki, na mwili wake unahifadhiwa katika makafani ukisubiri kufanyiwa upasuaji.
Awali, misa ya wafu kwa ajili ya jaji Majanja imefanyika jijini Nairobi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa