#Business

WABUNIFU KUNUFAIKA NA MSWADA WA USAIDIZI WA UCHUMI BUNIFU

Makundi ya watu wabunifu,  pamoja na wasanii na wacheshi wanaotumia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii, wanatazamiwa kufaidika na Mswada wa wa Uchumi Ubunifu wa 2023, ambao hutoa usaidizi kwa watu katika tasnia ya ubunifu.

Mswada huo uliopendekezwa na Seneta wa Migori Eddy Gicheru Oketch mwaka wa 2023 unalenga kuanzisha hazina ya ubunifu ili kuimarisha michango ya sekta katika uchumi wa taifa.

Kulingana na seneta huyo, uchumi wa ubunifu hutumia ubunifu wa binadamu, uvumbuzi, na mawazo ili kukuza maendeleo ya kiuchumi.

Hazina hiyo itakuwa ya fedha ambazo zinaweza kugawiwa kwa hazina ya Bunge na misaada, michango, au tuzo nyinginezo.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *