MANCHESTER UNITED WALAZWA MABAO 3-1 NA BRIGHTON

Manchester United walizabwa mabao 3-1 na Brighton kwenye Uwanja wa Old Trafford, wakati wakimkumbuka gwiji wa klabu Denis Law, aliyefariki Ijumaa akiwa na miaka 84.
Yankuba Minteh alifunga bao la mapema kwa Brighton kabla ya Bruno Fernandes kusawazisha kupitia penalti. Kaoru Mitoma na Georginio Rutter walifunga mabao mengine, wakiiwezesha Brighton kupanda hadi nafasi ya tisa, huku United wakibaki nafasi ya 13.
Kabla ya mechi, wimbo wa “Flower of Scotland” ulipigwa kwa heshima ya Denis Law, mshindi wa Ballon d’Or na mfungaji wa tatu bora wa United katika historia.
Imetayarishwa na Janice Marete