WALIMU WA CHEKECHEA WALALAMIKIA AJIRA MIEZI MBILI BAADA YA KUPEWA KANDARASI YA KUDUMU
Walimu wa shule za chekechea katika kaunti ya Pokot Magharibu wameibua lalama miezi miwili tu baada ya gavana wa kaunti hiyo Simon Kachapin kuwapa kandarasi ya kudumu.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa muungano wa walimu wa chekechea katika kaunti hiyo Joseph Sarich kndarasi walizopewa walimu hao haziendani na kanuni zilizowekwa na tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma SRC.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































