HOFU YA KUSITISHA SHEREHE ZA TAMADUNI YATANDA MIONGONI MWA VIJANA KAUNTI YA KAKAMEGA
Sherehe za michezo ya tamaduni ambazo hufanyika kila mwishoni mwa mwaka katika kaunti ya Kakamega zimeibua hisia kinzani huku baadhi ya wakazi wakisema hazitafanyika.
Vijana wanaoshiriki michezo ya sanaa wa kaunti hiyo wametoa wito kwa kaunti hiyo kupitia wizara ya michezo kuweka wazi tetesi zinazonezwa kwamba tamasha ya mashindano ya tamaduni inayoandaliwa kila mwaka haitakuwapo mwaka huu.
Vijana hao wameleza wasi wasi wao wakisema kwamba wamejitayarisha vya kutosha kushiriki michezo hiyo hivyo kutofanyika kwa michezo hiyo kutawakosea sana kwa kuwa michezo hiyo imewapa vijana wengi ajira.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































