#Sports

KENYA KUJIUNGA NA EBRD

Kenya inatazamiwa kuwa mwanachama wa Benki ya Ulaya ya Kujenga Upya na Maendeleo (EBRD) kufuatia kuidhinishwa kwa kauli moja na Bunge la Kitaifa, kuashiria hatua muhimu katika msukumo wa nchi wa kuimarishwa kwa maendeleo ya miundombinu na ukuaji wa uchumi.

Uidhinishaji huo unaweka Kenya kama nchi ya sita ya Afrika-baada ya Benin, Côte d’Ivoire, Ghana, Nigeria, na Senegal-kujiunga na mkopeshaji wa kimataifa kama mwanahisa.

Uanachama katika EBRD unatarajiwa kuipa Kenya fursa ya ufadhili wa masharti nafuu, hasa kwa miradi ya miundombinu na usaidizi kwa biashara ndogo ndogo na za kati (MSMEs), na hivyo kurahisisha utegemezi wa ukopaji wa gharama kubwa wa ndani.

Mwenyekiti wa Kamati ya fedha na mipango bungeni, Kimani Kuria, ambaye aliwasilisha hoja hiyo, amesisitiza thamani ya kimkakati ya ushirikiano huo.

Imetayarishwa na Maureen Amwai

KENYA KUJIUNGA NA EBRD

GOR YATIMUA BENCHI LOTE LA UFUNDI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *