#Local News

IKULU: HAKUTAKUWA NA KUPOTEZA AJIRA

Msemaji wa Ikulu, Hussein Mohamed, amesema hakuna mfanyakazi atakayepoteza kazi kufuatia uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa kuunganisha mashirika 42 ya kiserikali yenye majukumu yanayofanana kuwa mashirika 20.

Mageuzi hayo, yaliyotangazwa baada ya mkutano ulioongozwa na Rais William Ruto Kakamega, pia yanajumuisha kuvunjwa kwa mashirika tisa na marekebisho ya mengine ili kupunguza matumizi ya umma.

Hussein amesisitiza kuwa wafanyakazi wote wa mashirika yatakayoathiriwa watahamishiwa Utumishi wa Umma.

Mashirika kama hazina ya Vyuo Vikuu na Mamlaka ya Barabara za Vijijini yataunganishwa na mashirika yenye majukumu yanayofanana, huku mashirika tisa kama Bodi ya Uainishaji wa Filamu Kenya na LAPSSET yakivunjwa, na majukumu yake kurudishwa kwa wizara husika.

Aidha, mashirika 16, yakiwemo Numerical Machining Complex, yatauzwa au kufutwa, na mashirika sita kama Chuo cha Kenya Utalii yatapitia marekebisho kuboresha utendaji. Mashirika ya kitaaluma kama Baraza la Uuguzi hayatapokea tena mgao wa bajeti ya serikali.

Imetayarishwa na Janice Marete

IKULU: HAKUTAKUWA NA KUPOTEZA AJIRA

RUTO AWAKEMEA WANAOPINGA SHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *