#Rugby #Sports

TIMU YA RAGA YAPATA MFADHILI

Wachezaji magwiji wa raga nchini Kenya hapo jana  waliboresha ushirikiano wao na kampuni moja ya kamari  katika mkataba wa Sh2 Milioni ambao utaimarisha timu hiyo kabla ya kushindana na wenzao kutoka Uganda.

Tukio hilo litaleta pamoja mkusanyiko wa wachezaji mashuhuri wa raga ambao tayari wametoka jukwaani, na ambao tayari wako katika majukumu ya usimamizi na vilabu tofauti.

Mechi inayowakutanisha Nondies Legends wa Kenya na Uganda Vets pia inatarajiwa kufufua hisia za baadhi wa  magwiji wakubwa katika historia ya raga ya Kenya.

Kikosi cha mwaka huu kinajumuisha nguli wa Shujaa Collins Injera, Lavin Asego, George Mbaye, Oscar Sudi, Moses Mukabane na nahodha Eddie Omondi.

Watacheza mechi ya mkondo wa kwanza Juni 8 katika uwanja wa Kings Park Arena jijini Kampala.

Timu hiyo inaongozwa na nahodha mzoefu Oscar Osir, ambaye wakati wa hafla hiyo ambayo pia ilishuhudia uzinduzi wa jezi rasmi za michezo hiyo, aliwashukuru wadhamini kwa kunyoosha mikono yao huku akiendelea kuwa na furaha kabla ya mechi hizo mbili

Mwenyekiti wa Nondescript Auka Gecheo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Cecafa alipongeza ushirikiano huo akisema utaathiri vijana katika mchezo huo.

Mwaka jana, wababe hao wa Kenya walishinda 6-38 katika safari ya ugenini ya Uganda kabla ya kupata ushindi wa 31-12 nyumbani na kutwaa Kombe la Legends 2023.

Imetayarishwa na Nelson Andati

TIMU YA RAGA YAPATA MFADHILI

KFS NA MAAFISA WENGINE WAENDELEZA UPANZI WA

TIMU YA RAGA YAPATA MFADHILI

BANDARI WASHABIKIA WACHEZAJI IBUKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *