RAIS RUTO AENDELEA KUKWEA

Rais William Ruto ameendelea na ziara yake ya maendeleo kwa siku ya pili katika eneo la Mlima Kenya ambako amezindua miradi mbali mbali anayosema itasaidia kubadilisha Maisha ya wakazi wa eneo hilo.
Kaunti za Meru na Kirinyaga ni maeneo ambako Rais anazuru hii leo, akikariri kuwa urafiki wake na eneo hilo utasalia kuwa imara.
Rais ameandamana na naibu wake Kithure Kindiki na viongozi mbali mbali wa eneo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa