HOMA BAY YAANZISHA MIPANGO YA KUFUNFUA VIWANDA HUKO KARACHUONYO
Serikali ya kaunti ya Homa Bay inatayarisha mpango mkuu wa kuanzisha viwanda katika Eneo Maalum la Kiuchumi la Riwa katika eneo bunge la Karachuonyo.
Mpango huo unaandaliwa baada ya uchunguzi wa hali ya hewa kufanyika ili kuiwezesha serikali kuweka ramani na kutambua maeneo ambayo viwanda vitaanzishwa.
Serikali ya kaunti hiyo inashirikiana na mashirika mengine, Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA), Mamlaka ya Eneo Maalum la Kiuchumi (Seza), Tume ya Kitaifa ya Ardhi (NLC) na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (Nema) katika kuandaa mpango huo.
Hifadhi hiyo ya viwanda yenye ukubwa wa ekari 532 itakuwa na makampuni mbalimbali yanayofanya kazi kutoka eneo moja.
Gavana wa kaunti hiyo Gladys Wanga na maafisa kutoka mashirika tofauti ya serikali, walizuru eneo hilo.
Kwa mujibu wa Wanga kukamilika kwa Ukanda Maalum wa Kiuchumi wa Riwa kutaifanya Homa Bay kuwa kaunti ya kwanza katika kanda ya ziwa kuanzisha uwanja wa viwanda.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































