OILERS WAPONGEZWA LICHA YA KUPOTEZA FAINALI KWA KABRAS
Kocha mkuu wa timu ya raga ya Shule ya Upili ya Kakamega ameisifu Menengai Oilers kwa juhudi zao licha ya kupoteza kwa alama 27–26 dhidi ya Kabras RFC katika fainali ya Kenya Cup.
Kocha huyo, Wamanga, alisema ilikuwa mechi ngumu kwa mabingwa watetezi. Aliweka wazi kuwa anatarajia pambano kali zaidi katika fainali ya Kombe la Enterprise, itakayochezwa Jumamosi katika uwanja wa RFUEA.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































