KEPSHA: JSS IMETUONGEZA MZIGO, TUTAMBUENI
Muungano wa walimu wa shule za msingi KEPSHA umeitaka serikali kuwatambua kikamilifu walimu wakuu kufuatia majukumu wanayotekeleza ya usimamizi wa shule za sekondari msingi JSS.
Mwenyekiti wa muungano huo Johnson Nzioka amesema kwa sasa walimu hao wanakabiliwa na majukumu mengi baada ya shule hizo kuwekwa chini yao.
Nzioka ameyasema haya katika kongamano linaloendelea jijini Mombasa ambako viongozi wakuu serikalini akiwemo mkuu wa utumishi wa umma na Waziri wa elimu wanatarajiwa kuhudhuria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































