WATU TISA WAUAWA KATIKA MILIPUKO KATIKA GHALA LA RISASI CHAD

Watu tisa wameuawa na wengine 46 kujeruhiwa katika milipuko iliyosababishwa na moto katika ghala la silaha za kijeshi katika mji mkuu wa Chad jana usiku.
Kwa mujibu wa waziri wa afya Abdelmadjid Abderahim Idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka huku watu wengi wakipata majeraha mabaya.
Milipuko hiyo ilitanda angani usiku juu ya kambi ya kijeshi karibu na uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa wa taifa hilo la Afrika ya kati na kusababisha makombora kuruka katika nyumba za karibu ambapo wakaazi waliojawa na hofu walitatizika kutafuta mahali pa kujificha.
Imetayarishwa na Janice Marete