GAVANA MPYA WA MERU APISHWA

Isaac Mutuma M’Ethingia, ambaye amehudumu kama Naibu Gavana wa Kaunti ya Meru tangu mwaka wa 2022, sasa ameanza majukumu ya ugavana.
Hii inafuatia kuondolewa madarakani kwa Gavana Kawira Mwangaza kupitia mashtaka ya Bunge la Seneti mwaka wa 2024, hatua ambayo ilidhibitishwa na uamuzi wa mahakama mnamo Machi 14, 2025.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa Mutuma ameahidi kuleta maendeleo katikia kaunti hiyo.
Imetayarishwa na Janice Marete