#Local News

NZOWASCO YAVUNJWA KUPISHA NAFASI YA KUBUNIWA KWA KAMPUNI NYINGINE

Uamuzi wa kuvunjwa kwa kampuni ya kusambaza maji ya zowasko kaunti ya Transnzoia umeafikiwa baada ya kufanyika kwa mkutano wa mwaka .

Maafikiano haya ni baada kuidhinishwa kwa ripoti yha kufanikisha mchakato mzima wa kuvunjwa kwa kampun I hniyo ambayo imekuwa ikisambaza maji katika kaunti ya Transnzoia na Bungoma.

Waziri na afisa mkuu wa wizara ya maji, mazingira mali asili na tabia nchi katika kaunti hiyo Pepela Wanjala na Dorothy Nyukuri wanasema madhumuni ya kufanya hivyo ni kila kaun ti kubuni kampun I yake ili kuboresha huduma za kusambaza maji safi na salama ya kutumia kuimarisha ukusanyaji wa kodi na kubuni nafasi za ajira.

Meneja mkurugenzi mkuu wa zowasko Matthew Maruti amesema sheria itazingatiwa wakati wa kugawa mali hya kampuni hiyo bila kuwaachisha kazi wafanyakazi katika kampuni hiyo.

NZOWASCO YAVUNJWA KUPISHA NAFASI YA KUBUNIWA KWA KAMPUNI NYINGINE

MAHAMAKA YA MAVOKO IMECHOMEKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *