UPINZANI WASHINIKIZA MASHAURIANO NA RUTO
Viongozi wa upinzani wakiongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua na makamu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka wamemtaka Rais William Ruto kuwashirikisha kabla ya kuwateua makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.
Kupitia taarifa baada ya mkutano jijini Nairobi, viongozi hao wamesema mashauriano hayo yatahakikisha pande zoet zinaafikiana kuhusu orodha ya mwisho ya watakaoteuliwa.
Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Pamoja na Martha Karua, Eugene Wamalwa, Justin Muturi, Mithika Linturi, Fred Matiang’i na Torome Saitoti.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































