“HATUELEWANI, DAWA IKO!”- NAKURU
Naibu gavana wa Nakuru David Kones amekanusha madai ya ukosefu wa dawa katika vituo vya afya kwenye kaunti hiyo, akisema kuna utaratibu unaofuatwa katika kusambaza dawa katika kila hospitali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa dawa za zaidi ya shilingi milioni 26.2 kutoka kwa mamlaka ya usambazaji wa dawa nchini KEMSA, Kones amesema kuna baadhi ya aina ya dawa ambazo hupatikana tu katika viwango mbali mbali vya hospitali.
Aidha, ameiagiza wizara ya afya kuhakikisha mikakati ya kuwekwa kwa mfumo wa kidijitali ili kuzuia uwezekano wa wizi wa dawa katika hospitali za umma kaunti ya nakuru.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































