MATAIFA YA MAGHARIBI YAITAKA KENYA KUTAFUTA TATHMINI YA IMF KUHUSU MASUALA YA UFISADI
Wanahisa wakuu katika Hazina ya Fedha ya Kimataifa wanaitaka Kenya kuomba tathmini ya hazina ya IMF kuhusu ufisadi na masuala ya utawala kama sehemu ya msukumo wa kufungua mikopo ambayo imekwama kutokana na kupunguzwa kwa nyongeza ya kodi.
Utoaji wa takriban dola milioni 600 chini ya mpango wa IMF unaoisha mwaka ujao umesitishwa tangu serikali kuondoa dola bilioni 2.7 katika ongezeko la kodi baada ya maandamano makubwa.
Maandamano hayo, ambayo yalisababisha watu kupoteza maisha yao na mali kuharibiwa , yaliibua masuala ya rushwa na ufisadi, huku vijana waandamanaji wakilalamika kuwa ushuru wao unatumiwa kufadhili maisha ya kifahari ya wanasiasa.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































