WABUNGE WALALAMIKIA HUDUMA DUNI ZA SHA
Wabunge wameeleza wasiwasi kuhusu changamoto katika hazina ya Bima ya Afya ya Jamii (SHIF), wakilalamikia utendaji duni wa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA).
Mbunge wa Belgut, Nelson Koech, ameilaumu Wizara ya Afya na uongozi wa SHA kwa kushindwa kushughulikia matatizo hayo.
Mbunge wa Gatanga, Edward Muriu kwa upande wake amesema Wakenya wanadhulumiwa kwa kulipa viwango sawa vya kodi huku wakipata huduma zisizo sawa, akipendekeza kurejeshwa kwa NHIF.
Mbunge wa Kathiani, Robert Mbui vile vile amelalamikia changamto hizo akisema kuwa SHIF ilianzishwa kwa haraka bila maandalizi ya kutosha.
Kamati ya Afya ya Bunge imepewa jukumu la kushughulikia changamoto hizi huku mpango huo ukizidi kupingwa kwa kushindwa kugharamia matibabu ipasavyo. Wabunge pia wamehoji iwapo SHA inaingiliwa na Wizara ya Afya.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































