MIANYA KWENYE TAARIFA YA POLISI

Idara ya polisi imethibitisha kumkamata afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumjeruhi vibaya mchuuzi wa maski katikati mwa jiji la Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga dhuluma za polisi dhidi ya wananchi.
Kupitia taarifa, msemaji wa polisi Muchiri Nyaga amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na amri ya inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, huku akishutumu makundi ya wahalifu yaliyowahangaisha waandamanaji machoni pa maafisa wa polisi.
Hata hivyo, idara hiyo haijaweka wazi jina la afisa huyo wala kituo anakohudumu, ikiibua maswali iwapo afisa huyo amekamatwa.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa