#Local News

APOSTLE MANYURU APINGA MSWADA ‘WA MUNGATANA’

Mwenyekiti wa muungano wa makanisa ya Pentecostal Voice of Kenya PVK ambaye pia ni kiongozi wa kanisa la Jesus Teaching Ministry Apostle Peter Manyuru, ameelezea hofu kuhusiana na mswada wa kudhibiti makanisa nchini, akisema mswada huo utalemaza shughuli za kanisa iwapo utapitishwa.

Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi akiwa ameandamana na viongozi wengine wa muungano huo, Apostle Manyuru amepinga mswada huo uliowasilishwa na seneta wa Tana River Danson Mungatana, akisema unakiuka uhuru wa kuabudu.

Aidha, wamelalamika kwamba mswada huo unalenga kuharamisha mahubiri kwa kupendekeza faini ya shilingi milioni 10 au kifungo cha miaka 5 gerezani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

APOSTLE MANYURU APINGA MSWADA ‘WA MUNGATANA’

WAWILI MAHAKAMANI KWA UFUJAJI WA FEDHA WEST

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *