MZIGO WA KARO MLANGONI
Huenda wazazi wakagharamika zaidi katika ulipaji wa karo kutokana na uamuzi wa wizara ya elimu kupunguza mgao wa masomo kwa shilingi bilioni 22 kwenye bajeti ya mwaka wa 2025-26.
Akizungumza mbele ya kamati ya elimu bungeni, waziri wa elimu Julius Ogamba, amesema pengo hilo litazibwa na wazazi ili kufadhili elimu katika shule za msingi na upili nchini.
Ongezeko la karo litaashiria mwisho wa elimu ya bure iliyoanzishwa na Rais mstaafu marehemu Mwai Kibaki.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































