#Football #Sports

EMERGING STARS WAZIDI KUTAMBA

Timu ya Kenya ya vijana chini ya umri wa miaka 23, Emerging Stars, imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi Zambia na kupeleka taarifa kubwa ya nia ya kuwania Kombe la COSAFA 2024 lililoanza leo kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Bay huko Port Elizabeth, Afrika Kusini.

Mchezaji wa Gor Mahia Austin Odhiambo aliifanyia Emerging Stars mambo katika dakika ya nane alipofunga mkwaju wa penalti baada ya Patrick Otieno kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Nguvu ya ushambuliaji ya timu hiyo iliendelea kung’ara huku mshambulizi wa Posta Rangers, Patrick Otieno akifunga bao la pili dakika ya 18, na kuwaacha mabingwa hao wakipambana kupanda.

Ushindi huo uliifanya Kenya kumaliza siku ya ufunguzi wakiwa kileleni mwa Kundi B kwa tofauti ya mabao baada ya Zimbabwe kuwalaza Comoro 1-0 katika mechi nyingine iliyochezwa mapema siku hiyo.

Kocha mkuu wa Emerging Stars Ken Odhiambo aliipongeza timu hiyo kwa mwanzo mzuri dhidi ya Zambia.

Kenya itasafiri hadi Wolfson Stadium Jumapili Juni 30, kumenyana na Comoro saa 1 jioni EAT, kabla ya kucheza mechi yao ya mwisho ya kundi dhidi ya Zimbabwe Jumanne Julai, 2024 saa 1 jioni EAT.

Imetayarishwa na Nelson Andati

EMERGING STARS WAZIDI KUTAMBA

HATUA ZA KITAALAMU ZA KUKABILI MABADILIKO YA

EMERGING STARS WAZIDI KUTAMBA

UCHOVU ULICHANGIA BUNGOMA QUEENS KUSHINDWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *