#Local News

MWENYEKITI WA IEBC, MAKAMISHNA KUAPISHWA LEO

Jaji mkuu Martha Koome anatarajiwa kuongoza hafla ya kumwapisha mwenyekiti mpya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Erastus Ethekon na makamishna 6 hii leo, ili kuanza majukumu yao rasmi.

Hafla hiyo itafanyika chini ya siku moja baada ya Rais William Ruto kuwateua 7 hao rasmi na kuchapisha majina yao kwenye gazeti rasmi la serikali, baada ya mahakama kutupilia mbali rufaa iliyokuwa ikipinga uteuzi wao.

Kubuniwa kwa IEBC kutaiwezesha kuanzisha mipango ya chaguzi ndogo katika maeneo mbali mbali na uchaguzi mkuu ujao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MWENYEKITI WA IEBC, MAKAMISHNA KUAPISHWA LEO

BARAZA LA MAGAVANA LALAMIKIA MADENI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *