KARUA AIKOSOA SERIKALI KWA KUTOA KIPAUMBELE USALAMA WA VIONGOZI
Kinara wa chama cha Peoples Liberation Party, Martha Karua, ameikemea vikali idara ya usalama kwa kuharakisha uchunguzi wa kifo cha Mbunge wa Kasipul, Charles Were, huku visa vingine vingi vya mauaji dhidi ya Wakenya wa kawaida vikiendelea kupuuzwa.
Karua anasema hatua hiyo inaonesha kuwa serikali haijajitolea kikamilifu kuhakikisha haki kwa waathiriwa wote, bali inaelekeza juhudi zake kwa viongozi walioko mamlakani pekee.
Kathalika amemkosoa spika wa bunge la taifa Moses Wetangula kwa kushinikiza ulinzi zaidi kwa wabunge huku akitaka kuwepo kwa usawa wa usalama ka wakenya wote
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































