MAHAKAMA KUAMUA HATMA YA MASENGELI

Mahakama kuu inatarajiwa kutoa uamuzi muda wowote kuanzia sasa kuhusu iwapo itampa adhabu kaimu inspekta mkuu wa polisi Gilbert Masengeli kuhusiana na uamuzi wake wa kupuuza maagizo mara 7 yaliyomtaka afike mahakamani.
Hii ni baada ya rais wa zamani wa chama cha wanasheria LSK Nelson Havi kumwomba jaji Lawrence Mugambi ampe Masengeli kifungo cha miezi 6, huku wakili wa serikali Charles Mutinda akisema hakuna msingi wa kumfunga mkuu huyo wa polisi.
Mahakama imekuwa ikimtaka Masengeli kufika mbele yake ili kueleza waliko wakenya 3 waliotekwa nyara mwezi jana na watu wanoaminika kuwa polisi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa