MAAFISA 5 TRANS NZOIA KUFIKISHWA KORTINI
Maafisa 5 wa kaunti ya Trans Nzoia akiwemo mwakilishi wadi ya Sinyerere John Makhanu, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mjini Kitale hii leo baada ya kukamatwa nje ya mahakama ya Milimani jijini Nairobi hapo jana walipokuwa wakihudhuria kesi ya gavana George Natembeya.
Kwa mujibu wa idara ya polisi, maafisa hao wanashukiwa kuwafadhili wahuni walioharibu magari ya tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC wakati wa kukamatwa kwa gavana Natembeya wiki kadhaa zilizopita.
Kesi ya ya ufisadi dhidi ya gavana huyo itatajwa tarehe 16 mwezi huu baada ya kuahirishwa hapo jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































