#Football #Sports

GORDON ASEMA SHARTI ASHINDE KOMBE

Winga wa Uingereza Anthony Gordon ameweka malengo yake ya kushinda kombe akiwa na Newcastle baada ya kusaini kandarasi ya muda mrefu siku ya Jumanne.

Gordon alijiunga na Newcastle kutoka Everton Januari 2023 na amecheza mechi 74 akiwa na Magpies, akifunga mabao 15 na kutoa asisti 11.

Kiwango cha kuvutia cha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kilimfanya acheze kwa mara ya kwanza England msimu uliopita na pia nafasi katika kikosi cha nchi yake cha Euro 2024.

Sasa Gordon anataka kusaidia kikosi cha Eddie Howe kushinda taji lao kuu la kwanza tangu 1969 Inter-Cities Fairs Cup.

Tuzo kuu la mwisho la Newcastle nyumbani lilikuwa Kombe la FA la 1955.

Imetayarishwa na Nelson Andati

GORDON ASEMA SHARTI ASHINDE KOMBE

GOR MAHIA WAKO TAYARI KWA MCHUANO WAO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *