HARAMBEE STARS IFANYIWE MABADILIKO

Nahodha wa zamani wa AFC Leopards Charles Okwemba sasa anasema ni wakati wa kuwa na mabadiliko ya kizazi katika timu ya taifa ya kandanda Harambee Stars.
Okwemba amesema wachezaji wanaokuja katika timu za vijana wanahitaji kupandishwa katika timu ya wakubwa ili waweze kuonyeshwa zaidi na uzoefu unaohitajika kwa maendeleo.
Stars ilishindwa kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani baada ya kutoka sare ya 1-1 na Zimbabwe siku ya Ijumaa na mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa anaamini kuwa ni wakati wa kuanzisha mradi mpya kabla ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 ambapo Kenya watakuwa wenyeji pamoja na Uganda na Tanzania.
Wakati uo huo anataka wajumbe kuwapigia kura ‘viongozi wanaofaa ambao wana nia bora ya soka la Kenya moyoni mwao’ kabla ya uchaguzi ujao wa urais wa FKF unaopangwa Desemba 7.
Imetayarishwa na Nelson Andati