SPAIN WAJIKATIA TIKITI KWA 16 BORA
Uhispania ilifuzu kwa hatua ya 16 bora ya Euro 2024 hapo jana usiku baada ya kuifunga Italia 1-0 katika mchezo mkali uliohakikisha kwamba La Roja ingefuzu kama washindi wa Kundi B.
Bao la kujifunga la Riccardo mnamo dakika tisa baada ya muda wa mapumziko lilihakikishia uhisipania ushindi huo.
Timu ya Luis de la Fuente ina pointi sita kamili kileleni mwa kundi na itamenyana na Albania siku ya Jumatatu ikijua kwamba tayari iko katika raundi ya muondoano na inacheza kama mabingwa watarajiwa.
Hata hivyo yote hayajapotea kwa timu ya Luciano Spalletti, ambayo iko nafasi ya pili kwa pointi tatu, kwani sare na Croatia siku ya Jumatatu itatosha kuwahakikishia kufuzu nyuma ya Uhispania.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































