#Local News

KANJA AWAFUTA KAZI MAAFISA WAKUU CENTRAL

Maafisa wa polisi akiwemo OCS wa kituo cha Central jijini Nairobi na wale waliokuwa kwenye zamu wakati wa kifo cha mwanablogi Albert Ojwang aliyefariki akiwa kwenye seli za kituo hicho wamesimamishwa kazi, huku mamlaka ya kuchunguza utendakazi wa polisi IPOA ikianzisha uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha jamaa huyo.

Kupitia taarifa ya msemaji wa polisi Muchiri Nyaga, hatua hizo zimechukuliwa ili kufanikisha uchunguzi wa kina na haraka, kuhusiana na kifo hicho ambacho kimeibua shutuma dhidi ya idara ya polisi.

Kulingana na babake Meshack Ojwang, mwanawe wa pekee alikamatwa Jumamosi kaunti ya Migori kwa tuhuma za kumchafulia jina afisa mkuu wa serikali.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KANJA AWAFUTA KAZI MAAFISA WAKUU CENTRAL

IPOA YAANZISHA UCHUNGUZI NAROK

KANJA AWAFUTA KAZI MAAFISA WAKUU CENTRAL

UPINZANI WAPINGA ‘MIRADI NDANI YA MRADI’

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *