RAIS MSTAAFU UHURU KENYATTA ASISITIZA HAJA YA KUIMARISHA MAENDELEO YA USALAMA BARANI AFRIKA

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa haja ya kujenga taasisi imara kwa ajili ya maendeleo ya usalama barani Afrika.
Akihutubia Kozi ya 33 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Nigeria (NDC) mjini Abuja, Kenyatta ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kuanzisha mifumo thabiti ya ndani kama msingi wa ushirikiano wa kikanda unaostahimili.
Katika hotuba yake kuu, uhuru ametoa mafunzo sita muhimu kutokana na uzoefu wake, akizingatia jinsi taasisi imara zinavyowezesha maendeleo endelevu na usalama wa taifa.
Amesisitiza kuwa kuwekeza katika rasilimali watu kwa kutengeneza njia zinazofaa za kijamii na kiuchumi kwa vijana wetu ni muhimu ili kufikia uthabiti wa kitaasisi.
Pia amejadili jukumu la wanajeshi katika kusaidia usalama wa taifa huku wakiheshimu usimamizi wa kiraia.
Imetayarishwa na Janice Marete