SHABANA WAANGUKIA NYOTA
Timu ya Shabana FC imewasajili beki wa kulia Nicholas Meja na fowadi James Mazembe, kutoka kwa wapinzani wao Bandari FC na KCB mtawalia.
Katibu Mkuu Elizaphan Kerama amethibitisha kuwasili kwa wawili hao, na kufichua kuwa kesho watajiunga na wenzao katika uwanja wa Shule ya Upili ya Cardinal Otunga, kwa kambi ya mazoezi huko Mosocho.
Wiki iliyopita, klabu hiyo iliwasajili kiungo mshambuliaji Cliff Nyakeya na kipa Maxwell Mulili kutoka AFC Leopards.
Shabana wanataka kusajili zaidi ya wachezaji 10 katika dirisha hili la usajili baada ya kuachana na wachezaji 14, kulingana na Kerama.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































