AFUENI YA MASOMO WEBUYE EAST

Ni afueni kwa wanafunzi wa vyuo vya anuai na vile vya utabibu katika eneo bunge la Webuye Mashariki baada ya hazina ya ustawishaji eneo bunge hilo kuzindua basari ya shilingi milioni 5 kufadhili masomo yao.
Akizungumza baada ya kuzindua zoezi hilo afisini mwake mjini Webuye, mbunge wa eneo hilo Martin Wanyonyi amekariri kuwa fedha hizo zitawapunguzia mahangaiko ya kusaka karo.
Kauli yake imesisitizwa na mwakilishi wa wadi ya Maraka Ali Machani, akihimiza ushirikiano miongoni mwa viongozi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa