MGOMO WATATIZA UCHUKUZI KIRINYAGA
Shughuli za uchukuzi zimetatizika katika eneo la Kerugoya kaunti ya Kiriyaga, baada ya wahudumu wa matatu kugoma wakilalamikia hatua ya wamiliki wa magari ya kibinafsi kubeba abiria bila leseni.
Wahudumu hao wameapa kutorejesha magari yao barabarani hadi usimamizi wa kaunti hiyo utakapoingilia kati kutatua mgogoro huo.
Hata hivyo, maafisa wa polisi eneo hilo wamewataka wahudumu hao kurejelea shughuli zao wanaposhughulikia suala hilo
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































