KESI YA MBUNGE MBADI KUHUSU KUTUMWA KWA KDF KUAMULIWA LEO

Mahakama Kuu imetupilia mbali ombi la Mbunge wa Suba Kusini John Mbadi na wengine wawili kushiriki katika kesi iliyowasilishwa na Chama cha Wanasheria nchini Kenya kupinga kutumwa kwa maafisa wa kijeshi.
Mbadi, Dkt James Nyikal na Wilberforce Ojiambo walitaka kuruhusiwa kujiunga na kesi hiyo kama wahusika wakisema wana ufahamu wa kina kuhusu jinsi utumwa huo uliidhinishwa na kwamba walitazamia kutoa mtazamo wa ndani ambao kulingana nao ungesaidia mahakama kuamua ombi hilo.
Mahakama wakati huo huo imeruhusu muunganishi wa Kituo Cha Sheria na Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya hatua ambayo kulingana na jaji Mugambi ameazingatia kwamba ina jukumu la kukuza uzingatiaji wa haki za binadamu nchini.
Imetayarishwa na Janice Marete