MUUNGANO WA WAFANYIBIASHARA KAKAMEGA WAUNGA MKONO PENDEKEZO LA MBADI

Muungano wa wafanyibiashara Chamber of Commerce katika kaunti ya kakamega umeunga mkono pendekezo la Waziri wa fedha John Mbadi kurejesha baadhi ya vipengele muhimu katika mswada wa fedha 2024 uliotupiliwa mbali.
Mwenyekiti wa muungano huo Wycliffe Kibicu anasema kuwa baadhi ya vipengele hivyo vitasaidia kuimarisha uchumi na vile vile kulinda taifa dhidi ya kuwa eneo la kutupa bidhaa ambazo hazitumiki katika mataifa mengine.
Imetayarishwa na Janice Marete