#Local News

POLISI KUONGEZWA BILIONI 29

Wizara ya usalama wa kitaifa imesema kwamba serikali imeongeza mgao wa shilingi bilioni 29.4 kwa idara ya polisi katika mpango wake wa kuboresha mazingira ya utendakazi wa maafisa wa polisi katika kipindi cha miaka 3 ijayo.

Kupitia taarifa, wizara hiyo imesema fedha hizo zitatumika kwa ununuzi wa vifaa vya kisasa yakiwemo magari na helikopta kwa lengo la kukabili ugaidi na ujangili hasa katika maeneo ya kaskazini mwa bonde la ufa.

Kwenye bajeti ya mwaka huu wa kifedha, wizara ya usalama wa kitaifa imetengewa shilingi bilioni 110, bilioni 11 zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

POLISI KUONGEZWA BILIONI 29

BUNGE LA BUNGOMA LAWACHUNGUZA MAWAZIRI WAWILI

POLISI KUONGEZWA BILIONI 29

KNUT SASA YAILILIA SERIKALI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *