DIG LAGAT KUREJEA KAZINI LEO
Naibu inspekta mkuu wa polisi aliyejiondoa kwa muda Eliud Lagat ameratibiwa kurejea kazini hii leo baada ya ripoti ya uchunguzi kukosa kumpata na ushahidi unaomhusisha moja kwa moja na mauaji ya mwalimu na bloga Albert Ojwang.
Walio karibu na Lagat waliwadokezea wanahabari kwamba Lagat amechukua uamuzi wa kurejea kazini baada ya vitengo vyote vya uchunguzi kumwondolea lawama.
Haya yanajiri huku jaji Chacha Mwita akitarajiwa kutoa mwelekeo katika kesi ambapo mwanaharakati Karanja Matindi, aliyepinga uamuzi wa Lagat kujiondoa kazini kwa muda.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































