#Local News

ONG’ONDO: MSHUKIWA MKUU KUWASILISHWA JKIA

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Ong’ondo Were, Isaac Kuria aliyekamatwa hapo jana katika eneo la Isebania, ameratibiwa kuwasilishwa katika mahakama ya JKIA majira ya 2pm ambapo polisi wanatarajiwa kuomba muda zaidi wa kuendelea kumzuilia wanapoendesha uchunguzi.

Kuria anayeaminika kufyetua risasi iliyomuua Ong’ondo, alikamatwa akiwa mafichoni, polisi wakikisia kwamba alikuwa na njama ya kutorokea nchi Jirani ya Tanzania.

Mahakama tayari imeamuru mshukiwa mwingine Philp Aroko azuiliwe kwa siku 7 zaidi, jumla ya washukiwa 11 wakiwa kizuizini kuhusiana na mauaji hayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

ONG’ONDO: MSHUKIWA MKUU KUWASILISHWA JKIA

USHIRIKIANO WA KENYA-FINLAND

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *