JESHI LA SUDAN LAAPA KUISAMBARATISHA RSF
Mkuu wa Jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, amekataa maridhiano na RSF, akiapa kuisambaratisha.
Hata hivyo, amesema wapiganaji wanaojisalimisha na kuweka silaha chini wanaweza kusamehewa.
Jeshi limedhibiti Soko Libya, eneo muhimu Omdurman, na kudai ushindi Khartoum huku vita hivyo vya miaka miwili vikisababisha baa la njaa na mzozo mbaya wa kibinadamu, na kupelekea zaidi ya watu milioni 12 kukimbia makazi yao.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































