DP GACHAGUA KUHUTUBIA TAIFA USIKU WA LEO KAMA SAA YA KUONDOLEWA MADARAKANI IKIKARIBIA

Naibu Rais Rigathi Gachagua anatazamiwa kufanya kikao na wanahabari jioni ya leo, saa chache kabla ya hoja yake ya kuondolewa madarakani kujadiliwa katika Bunge la Kitaifa.
Ofisi ya Gachagua imetuma mwaliko kwa vyombo vya habari, ikisema kuwa anwani itakuwa katika makazi yake rasmi huko Karen mwendo wa saa moja.
Hotuba inayotarajiwa inajiri wakati ambapo Gachagua anakabiliwa na kung’olewa mamlakani kwa misingi ya kugawanya Wakenya kwa misingi ya kikabila, kuhujumu urais, kukiuka kiapo cha afisi na kukinzana na Sheria ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa.
Imetayarishwa na Janice Marete