#Local News

MAKADIRIO YA IEBC

Tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC imependekeza kutengewa shilingi bilioni 57 ili kufanikisha uchaguzi mkuu ujao na chaguzi nyingine ndogo katika maeneo mbali mbali nchini.

Kulingana na mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Gitonga Murugara, IEBC inapanga kutumia shilingi milioni 788 kati ya shilingi bilioni 9.6 za mwaka ujao wa kifedha, kuandaa changuzi ndogo, makadirio zaidi yakitumika kununua vifaa vya kupigia kura.

Aidha, amesema tume hiyo inalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni 6.3 ili kuongeza kwenye idadi ya wapiga kura milioni 22.1 ya sasa kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *