MASOMO YASITISHWA NAKURU HIGH BAADA YA GHASIA ZA WANAFUNZI

Masomo katika Shule ya Upili ya Nakuru yamesitishwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kuandamana usiku wa kuamkia leo na kuharibu mali ya shule kutokana na malalamiko kuhusu chakula.
Ghasia zilianza saa 8 usiku na kudumu kwa takribani saa sita kabla ya polisi kuingilia kati. Wanafunzi waliharibu madarasa, mabweni, na jengo la utawala, huku wengine wakivamia ukumbi wa chakula na kuhifadhiwa.
Sababu kuu za maandamano zilihusisha kuondolewa kwa chai na mkate kwenye ratiba ya asubuhi, mfumo mpya wa kulipia bidhaa kwa kadi badala ya pesa taslimu, na kucheleweshwa kwa uboreshaji wa vifaa vya burudani licha ya michango yao.
Utulivu ulirejea baada ya polisi na Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti ya Nakuru, Victoria Mulili, kuingilia kati.
Imetayarishwa na Janice Marete