#Sports #Tennis

ANGELA OKUTOYI AZIDI KUTAMBA

Bingwa mtetezi wa michezo ya Afrika, Angela Okutoyi aliongoza kikosi cha Kenya dhidi yawashindi wa fainali za mwaka jana Tunisia kuendeleza matokeo mema katika Kundi B, huku Kenya ikiimarisha matarajio yao ya kupanda daraja katika siku ya pili ya Kundi la Tatu michuano ya Billie Jean King Cup katika Klabu ya Nairobi.

Kenya ilianza vibaya huku Cynthia Cheruto akishindwa kwa seti za 6-2, 6-4 dhidi ya Ranim Rassil wa Tunisia katika mchezo wa ufunguzi kabla ya Okutoyi kumzaba Chiraz Bechri 6-3 na 7-6.

Alafu Okutoyi bingwa wa Junior Wimbledon mara mbili aliungana na Cynthia Cheruto katika mchezo wa tatu na kuwazidi nguvu washiriki wawili wa Tunisia Chiraz Bechri na Rassil Ranim kwa seti za 6-2, 6-3 na kuipa Kenya ushindi wa 2-1 dhidi ya waafrika Kaskazini hao.

Hii leo Kenya imeratibiwa kucheza mchezo wao wa mwisho wa kundi B dhidi ya Burundi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

ANGELA OKUTOYI AZIDI KUTAMBA

BARONI ACHUKUA USUKANI LAZIO

ANGELA OKUTOYI AZIDI KUTAMBA

SAFARI YA HARAMBEE STARS YAZIDI KUDIDIMIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *